Government Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Historia

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (Tume) ilianzishwa Mwaka 1980 kwa Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Sura ya 171 kama Idara ya Serikali inayojitegemea. Hata hivyo Tume ilianza kazi rasmi  tarehe 21 Oktoba,1983.

Historia ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ilianza Mwaka 1974 , ambapo Serikali iliunda Tume ya Kupitia Mfumo wa Sheria (Judicial System Review Commission) kwa lengo la kubaini changamoto katika mfumo wa usimamizi wa haki nchini na kupendekeza namna ya Kuuboresha.Tume hiyo ilijulikana kwa jina la Tume ya Msekwa, ikibeba Jina la Pius Msekwa aliyekuwa mwenyekiti na aliwasilisha Taarifa hiyo Mwaka 1977.

Katika Taarifa ya Tume, pamoja na mambo mengine, ilibaini  umuhimu wa kuwa na mpango wa muda mrefu utakaohakikisha kuwa Sheria zinazofanyiwa mapitio ili ziende sanjari na uhalisia wa mabadiliko ya kijamii, Kiuchumi, Kiteknolojia na Kisiasa. Pendekezo hili lilitokana na tafiti zilizofanyika kwenye nchi za Australia, Canada, Papua New Guinea, Zambia na Nigera hizi ni nchi ambazo zilikuwa na Taasisi mahsusi za kupitia Sheria mara kwa mara. Tume ya Msekwa ilipendekeza kuanzishwa kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ikiwa na jukumu la kufanya mapitio ya Sheria nchini na kupendekeza Serikalini Marekebisho yanayohitajika