Kinaongozwa na (Mkaguzi Mkuu) - Florent Mwenda
i.Kuandaa mpango kazi wa mwaka wa ukaguzi kulinga na njia sahihi yakukabiliana na Viashiria hatarishi na kuuwasilisha katika Kamati ya Ukaguzi kwa ajili ya kuipitisha na nakala kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
ii.Kutekeleza Mpango kazi wa Ukaguzi ulioidhinishwa pamoja na kazi maalumu au miradi kama itakavyoelekezwa na Kamati ya Ukaguzi, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali au Mwenye mamlaka husika.
iii.Kutoa muhutasari wa taarifa za vipindi za matokeo ya kazi za ukaguzi kwa Menejimenti, Kamati ya Ukaguzi na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali
iv.Kusaidia upelelezi wa shughughuli zenye hisia kubwa ya udanganyifu katika Wizara na kuitaarifu kamati ya Ukaguzi na Menejimenti
v.Kuweka utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyo katika taarifa za ukaguzi
vi.Kuisaidia menejimenti kufuatilia taarifa na mapendekezo yayamkaguzi wa Nje au Mamlaka ya uthibiti.
vii.Kufanya uhakiki maalum kama itakavyoelekezwa na Menejimenti au kamati ya Ukaguzi au Mkaguzi wa Ndan Mkuu wa Serikali
viii.Kuhakikisha kazi za ukaguzi ziko katika Miongozo na Misingi ya kitaaluma ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Ndani na viwango vinavyotumika vya taaluma ya ukaguzi wa ndani.
ix.Kuanzisha mpango wa kuhakiki ubora
x.Kuwa na wakaguzi wenye ufahamu wa ukaguzi wa kutosh
xi.Kuhakiki na kutoa Taarifa ya shughuli au program kama zinalingana na Malengo yaliyowekw
xii.Kufanya Ukaguzi na tathmini ya Maendeleo ya Miradi