Ununuzi na Ugavi
Majukumu ya Kitengo cha Ugavi na Ununuzi
Mkuu wa Kitengo - Nessy E. Kyejo
Kusimamia ununuzi wowote na uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni isipokuwa usuluhishi na kutunuku zabuni ;
Kuratibu shughuli za Bodi ya Zabuni ya Wizara;
Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya Wizara;
Kufanya kazi kama Sekritarieti ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
Kuandaa mpango wa Ununuzi na Uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni;
Kupendekeza ununuzi na uondoshaji wa mali za Wizara kwa utaratibu wa zabuni;
Kukagua na kuainisha upungufu wa mahitaji katika Wizara na kutoa tamko kuhusu mahitaji hayo;
Kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili wazabuni kushiriki;
Kuandaa matangozo ya fursa za zabuni;
Kuandaa rasmu za Mikataba;
Kutoa mikataba iliyothibitishwa na kusainiwa;
Kuandaa na kuhifadhi kumbukumbu za mchakato wa ununuzi na uuzaji wa mali za Wizara;
Kuandaa na kutunza orodha au kitabu cha mikataba yote ambayo Wizara imetunuku;
Kuandaa taarifa za kila mwezi kwa ajili ya Bodi ya Zabuni ya Wizara;
Kuandaa taarifa ya kila robo ya mwaka juu ya utekelezaji wa mpango wa ununuzi na kuwasilisha katika kikao cha menejimenti ya Wizara;
Kuratibu kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za serikali katika Idara na vitengo vyote vya Wizara; na
Kuandaa taarifa nyinginezo kadri zitakavyo hitajika muda wowote.