Government Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

Miradi inayoendelea

MIRADI INAYOENDELEA

  1. Mapitio ya Sheria Zinazosimamia Matumizi ya Bidhaa za Tumbaku ili Kudhibiti Matumizi ya Shisha na Sigara za Elektroniki  Tume ya Kurekebisha Sheria inafanya Mapitio ya Sheria zinazosimamia matumizi ya Bidhaa za Tumbaku ili kudhibiti matumizi ya Shisha na Sigara za kielektroniki. Mapitio haya yamejikita kuangalia sheria zinazosimamia matumizi ya bidhaa za tumbaku kwa kuzingatia kuwa matumizi ya shisha na sigara za kielektroniki yanahusisha bidhaa za tumbaku. Hivyo, mapitio haya yanalenga kubaini upungufu uliopo katika mfumo wa sheria zinazosimamia bidhaa za tumbaku na kuziboresha ili kudhibiti (kuweka utaratibu) matumizi ya Shisha na Sigara za kielektoniki.
  2. Mapitio ya Sheria ya Usuluhishi, Sura 15  Tume inafanya Mapitio ya Sheria ya Usuluhisho kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo katika utekelezaji wa sheria hiyo ili kutoa mapendekezo kwa Serikali hatua stahiki kwa kuhakikisha migogoro ya kibiashara inatatuliwa kwa haraka na kurahisisha ufanyaji wa biashara
  3. Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura ya 41 Tume inaendelea na Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Michezo ya Kubahitisha, Sura ya 41 ili kubaini iwapo malengo ya kutungwa kwa sheria hiyo yamefikiwa. Lengo la kufanya tathmini hii ni kuangalia ni kwa namna gani, pamoja na masuala mengine, watoto walio chini ya miaka 18 wanalindwa ili wasiingie katika michezo hiyo na kupata uraibu kutokana na ushiriki wao. Hivyo, Tume inajielekeza katika kutathmini mifumo ya usimamizi katika kulinda makuzi na maslahi ya mtoto ili michezo hiyo isiathiri ustawi wa jamii.
  4. Utafiti wa Mfumo wa Sheria zinazosimamia adhabu  ya kifo na Mifungo cha maisha
  5. Utafiti wa mfumo wa Sheria zinazosimamia utatuzi wa migogoroya mikopo katika benki na Taasisi za Fedha zinazosimiwa na benki kuu