Kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, wanawake kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imetoa msaada wa mahitaji mbalimbli Katika Kituo cha wasioona watu wazima Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodom Naibu katibu mkuu tume ya kurekebisha sheria Zainabu Chanz amesema wao kama wakinamama wameona ni vyema kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji hao ikiwemo Mchele Kg100, Maharage Kg100, Mipira ya kumwagilia maji 2, Unga sembe Kg100, Chumvi Pisi 80, Mafuta ya kula Lita 40, Sabuni za Unga mifuko 2 sawa na pisi 60 Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo hicho Mzee Yaledi Chereso amesema kuwa kituo hicho Wanaishi kwa kujitegemea wenyewe na misaada kutoka wa wadau mbalimbali hivyo kwa ujio wao umeleta matumaini ma faraja katika kituo hivyo Aidha Mzee Chereso ametoa ombi kwa tume hiyo kuwapatia elimu ya sheria kutoka kwa wataalamu hao ili kujua haki zao za msingi kama walemavu kwani kwakufanya hivyo kutaleta mshikamano na kupinga ukatiki wa kijinsi Vumilia Sara Mgandu mmoja wa wanaoishi katika kituo hicho ameeleza kuwa ingawa anasumbuliwa na ulemavu wa macho lakini anajishughulisha na utengenezaji wa sabuni za maji, kuku na ndizi (Ujasiriamali) hivyo ameshukuru kwa misaada hiyo ikiwemo kumuungisha bidhaa zake,